Kaunti ya Nairobi inaongoza kwa kuandikisha idadi kubwa ya watu waliojitokeza kupata chanjo dhidi ya corona ya AstraZeneca.

Takwimu kutoka kwa wizara ya afya zinaonesha kwamba watu (198,808) wamepata chanjo hiyo Nairobi, ikifuatiwa na Nakuru ambapo watu (34,682) wamepata chanjo hiyo,

Uasin Gishu ni ya tatu, (31,503), Kiambu ni ya nne (30,176) huku Nyeri ikifunga tano bora kwa kuwachanja watu (21,845).

Kaunti ambazo zina idadi ndogo ya watu waliochanjwa ni; Lamu 451, Marsabit 462, Tana River 633, Mandera 1,209 na Isiolo 1,377.

Kitaifa, katibu mkuu katika wizara ya afya Dkt. Rashid Aman anasema watu waliopata chanjo hiyo ni 616,166.