Mamlaka ya kumulika utendakazi wa Polisi (IPOA) imeanzisha uchunguzi kuhusiana na tukio ambapo kijana mmoja anadaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na Polisi katika eneo la Mountain View Kabete, kaunti ya Kiambu.

Familia ya marehemu Nicholas Lifede inasema mwanao alikuwa anaingilia kati kumtetea dadake mdogo aliyekuwa anadhulumiwa na Polisi Alhamisi iliyopita ya Aprili 8.

IPOA kupitia taarifa iliyotumwa na mwenyekiti wake Anne Makori inasema imewatuma maafisa wake katika eneo la tukio kufanya uchunguzi kubaini ni vipi kijana huyo aliuawa.

Tume hiyo baadaye itatoa ripoti yenye mapendekezo pindi uchunguzi huo utakapoisha.