Seneta mteule wa Garissa Abdulkadir Haji anatazamiwa kuapishwa rasmi asubuhi hii kwenye kikao maalum cha bunge la Senate kilichoitishwa na spika Ken Lusaka.
Tume ya uchaguzi IEBC ilichapisha jina la Haji kuwa seneta wa Garissa kumrithi babake marehemu Yusuf Hajji aliyefariki mapema mwaka huu.
Haji alichaguliwa pasipo kuandaliwa kwa uchaguzi baada ya kukosekana kwa yeyote wa kumpinga.
Kikao hicho maalum vile vile kinatazamiwa kuangazia mswada wa ugavi wa mapato uliowasilishwa kutoka kwa bunge la kitaifa juma lililopita.