Mtahiniwa, 17, wa mtihani wa kidato cha nne KCSE unaoendelea amefariki baada ya kudungwa kisu mara kadhaa na mpenziwe, 27 huko Kitui.
Polisi katika eneo la Kisasi wanasema mshukiwa alikamatwa akijaribu kujiua baada ya kutekeleza mauaji hayo.
Mshukiwa ambaye alipata majeraha ya shingo na tumboni alikimbizwa katika hospitali ya Kitui Level 4 kwa matibabu akisubiri uchunguzi na kushtakiwa.
Polisi wanasema kifaa kilichojaa damu na kinachoaminika kutekeleza mauaji hayo kilipatikana katika eneo la tukio.