Waziri wa elimu Profesa George Magoha amewaondolea wazazi wasiwasi kwamba huenda shule zitakosa kufunguliwa kama ilivyopangwa kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya corona.

Akizungumza alipoongoza ufunguzi wa kuonteina ya mtihani wa kidato cha nne KCSE huko Kiambu, Profesa Magoha amesema upo uwezekano wa kupungua kwa maambukizi mapya ya corona na hivyo kalenda ya masomo haitahitilafiwa.

Waziri Magoha vile vile amesema wamezima njama zozote za kuiba mtihani huo na waliojaribu kufanya hivyo waligunduliwa mapema na kukamatwa.

Na huku maeneo mengi yakishuhudia mvua, waziri wa elimu amesema wanashrikiana na wizara ya usalama wa ndani hakikisha kuwa mtihani huo umefikakwa muda na watahiniwa wamekalia mtihani wao kama ilivyopangwa.