Kenya imeripoti maambukizi mapya 1,091 ya corona kati ya sampuli 7,300 zilizopimwa katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita na kufikisha 144,154 idadi ya maambukizi hayo nchini.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe ametangaza kuwa watu 533 zaidi wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi hiyo kuwa 98,183 huku maafa 17 zaidi yakidhibitishwa na kufikisha idadi hiyo kuwa 2,309.

Miongoni mwa waliofariki ni wazee 11 walio na umri wa miaka 60 na zaidi na kufikisha 1,100 idadi ya watu hao waliofariki kufikia sasa.

Wagonjwa waliolazwa katika hospitali mbalimbali ni 1,605 huku wengine 4,233 wakishughulikiwa nyumbani.

Idadi ya wagonjwa waliolazwa katika chumba cha watu mahututi ni 236 wengine 159 wakisaidiwa na mashine kupumua.

Kuhusu shuguhli ya utoaji chanjo ya Astrazeneca inayoendelea kote nchini, waziri Kagwe ametangaza kuwa jumla ya watu 422,021 wamepata chanjo hiyo ikiwemo wahudumu wa afya 110,523, maafisa wa usalama 34,150, walimu 59,906 na watu walio na umri wa miaka 58 na zaidi 217,442.

Miongoni mwa waliochanjwa ni wanaume 238,522 (56.5%) na wanawake 183,499 (43%).