Matokeo ya mtihani wa kitaifa wa darasa la nane KCPE yanatarajiwa kutolewa chini ya majuma mawili yajayo.

Waziri wa Elimu Profesa George Magoha amesema zoezi la usahihishaji liko karibu kutamatika na wanafunzi watafahamu matokeo yao hivi karibuni.

Watahiniwa 752,437 walikalia mtihani huo katika 10,437 kote nchini.

Mtihani huo ulifaa kufanyika Novemba mwaka uliopita umechelewa kutokana na janga la COVID19 ambalo lilitahiri kalenda ya masomo.

Kuhusiana na mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KCSE unaoendelea, waziri Magoha amewaonya wasimamizi wa mitihani hiyo dhidi ya kuwatuma nyumbani wanafunzi wanaopatikana wakijaribu kushiriki udanganyifu.