Bunge la kaunti ya Nairobi limehairisha vikao vyake kwa muda usiojulikana baada ya kuandikisha maambukizi mengi ya visa vya ugonjwa wa corona.

Akidhibitisha hili, spika wa bunge hilo Benson Mutura amesema madiwani wapatao 50 wamepatwa na virusi hivyo kufikia sasa.

Amesema 35 kati yao wamepona ugonjwa huo, wanne wangali wamelazwa huku wengine wawili wakitumia mashine kupata hewa.  

Spika Mutura amesema wengine waliopatwa na virusi hivyo wanaendelea kushughulikiwa nyumbani.