Watu wenye umri wa miaka 58 na zaidi wameongezwa kwenye orodha ya waliopewa kipau mbele kupokea chanjo ya corona kwenye awamu hii ya kwanza.

Katika taarifa, kamati inayosimamia utoaji wa chanjo hiyo kupitia mwenyekiti Dr. Willis Akhwale imesema kuwa watu hao wako katika hatari kubwa zaidi ya kukutwa na virusi hivyo na wengine wana magonjwa mengine ambayo yanahatarisha maisha yao.

Dr. Akhwale amesema asilimia 60% ya maafa zaidi ya alfu mbili ya corona yaliyoripotiwa nchini kufikia sasa ni ya watu walio na umri wa miaka 58 na zaidi.

Wizara ya afya vile vile inatoa wito kwa kwa viongozi wa kisiasa na wale wa kidini kuwa katika mstari wa mbele kupata chanjo hiyo ili kuwapa Wakenya motisha ya kuipata bila kuwa na wasiwasi.

Chanjo hiyo aina ya Astrazeneca inaendelea kutolewa kwa watu mbalimbali wakiwemo wahudumu wa afya, walimu na maafisa wa usalama.

Kenya kwa inashuhudia wimbi la tatu ya ugonjwa huo na idadi ya maambukizi na maafa inazidi kuongezeka.