Mwanahabari Robin Njogu aliyefariki baada ya kupatwa na ugonjwa wa corona atazikwa Jumamosi hii huko Cheranganyi kaunti ya Trans Nzoia.

Familia pamoja na marafiki wachache wa karibu wataruhusiwa kuhudhuria mazishi hayo kuambatana na muongozo uliotolewa na wizara ya afya kuzuia msambao wa virusi vya corona.

Hadi kifo chake, Njogu ambaye ibada ya wafu imeandaliwa katika kanisa la All Saints Cathedral alikuwa anafanya kazi na shirika la Royal Media Services.

Tasnia ya uanahabari, rais Uhuru Kenyatta pamoja na viongozi mbalimbali wamemtaja marehemu kama mwanahabari aliyekuza vipaji vingi na aliyezingatia maadili mema katika utendakazi wake.

Wanahabari wengine waliofariki kutokana na corona ni Reuben Githinji, Lorna Irungu na Winnie Mukami.