Bunge linamtaka rais Uhuru Kenyatta kurejesha marufuku ya kutotoka au kuingia kwenye baadhi ya kaunti kufuatia kuongezeka kwa maambukizi ya ugonjwa wa corona nchini.

Kamati ya bunge kuhusu afya chini ya uenyekiti wake mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Murang’a Sabina Chege inahoji kwamba kurejeshwa kwa marufuku hiyo kutasaidia kupunguza msambao huo haswaa wakati huu ambapo shule zimefungwa na sherehe za Pasaka zinakaribia.

Huku akihimiza wahudumu wa afya kujitokeza kupata chanjo ya corona, Chege amesema hatua zilizochukuliwa na serikali mwaka jana zilisaidia pakubwa na ni wakati wa kurejesha baadhi ya mikakati hiyo ili kusaidia katika kupambana na janga hilo.