Mwanahabari wa gazeti la The Star Reuben Githinji amefariki kutokana na matatizo yanayoambatana na virusi vya corona.

Akithibitisha kifo hicho, dadake Grace Wacheke amesema mwanahabari huyo, 52 amefariki akipokea matibabu katika hospitali ya Murang’a.

Githenji alianza kuugua wiki jana na kukimbizwa hospitalini ambapo alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).

Baraza la vyombo vya habari (MCK) limemuomboleza marehemu ambaye atazikwa nyumbani kwake Nyahururu.

Githinji ni mwanahabari wa pili kufariki wiki hii kutokana na corona baada ya Lorna Irungu huku Robin Njogu na Winnie Mukami wakifarki kutokana na ugonjwa huo juma lililopita.