Bodi ya Famasia nchini Kenya imeidhinisha kuanza kutumika kwa chanjo ya Sputnik V kutuka Urusi katika juhudi za kupambana na virusi vya corona.

Bodi hiyo inasema chanjo hiyo imeidhinishwa kutumika baada ya awamu zote tatu kuonyesha kuwa chanjo hiyo ni salama na haina madhara kwa binadamu.

Bodi hiyo ambayo inahusika na kuchunguza usalama wa dawa nchini pia ilihalalisha chanjo ya Astrazeneca ambayo inaendelea kutumika nchini kwa sasa.

Kenya inaendelea kurekodi idadi kubwa ya maambukizi na maafa katika awamu hii ya tatu ya ugonjwa wa corona.