Madaktari 10 wamelazwa katika hospitali mbalimbali nchini baada ya kuambukizwa virusi vya corona.

Muungano wa madaktari nchini KMPDU kupitia kaimu katibu Dr Chibanzi Mwachonda unasema hali hiyo inasikitsha na kuelezea kwamba kuongezeka kwa maambukizi hayo nchini huenda kukalemea zaidi sekta ya Afya ambayo kwa sasa inajizatiti kuhudumia wagonjwa wengi wanaopatwa na corona.

Muungano huo pia umeitaka serikali kuweka mbele maslahi ya wahudumu wa Afya wanaopambana na virusi hivyo na pia kuongeza mkataba wa wahudumu wa afya 156 walioajiriwa kwa kandarasi kuhudumu katika vituo vya karantini.

Wakati uo huo madaktari hao wanasema wanaunga mkono utoaji wa chanjo ya corona ya Astrazeneca na kudokeza kua wanalenga kuanzisha kampeni ya kuwasihi Wakenya kukubali kuipokea.