Agnes Kavindu Muthama ameapishwa rasmi kuwa Seneta wa Machakos baada ya kushinda uchaguzi mdogo wa Alhamisi iliyopita.

Kavindu aliyeshinda kiti hicho kwa tiketi ya chama cha Wiper ameapishwa Jumanne alasiri na spika wa bunge la Senate Kenneth Lusaka.

Kavindu alitangazwa mshindi baada ya kupata kura 104,080 akifuatiwa kwa umbali na Urbanus Ngengele wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) kwa kura 19,705.

Kiti hicho kilisalia wazi baada ya kifo cha senata Bonface Kabaka Disemba mwaka jana.