Wagonjwa zaidi 12 wamefariki kutokana na virusi vya Corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi ya maafa nchini kuwa 2,023.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amedhibitisha kuwa watu 1,130 wamekutwa na ugonjwa huo baada ya sampuli 5,119 kupimwa na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 122,040.

Idadi ya waliopona imeongezeka na kufika 90,376 baada ya wagonjwa 754 kupona.

Wagonjwa 121 wamelezwa katika vyumba vya watu mahututi (ICU).