Kwa mara nyingine maafisa wa polisi wamewataka wakenya kutoabiri magari ambayo hayafuati masharti ya kujikinga na virusi vya Corona.

Inspekta Jenerali Hillary Mutyambai kupitia kwa ukurasa wake katika mtandao wa Twitter kuwa ni jukumu la kila mmoja kufuata masharti ili kujikinga kutopatwa na virusi hivyo.

Mutyambai vilevile amewasihi maafisa wa polisi kuendelea kushika doria na kuwachukulia hatua wanao kiuka sheria hizo haswa magari ya uchukuzi wa umma yanayobeba abiria kupita kiasi.