Samia Suluhu Hassan ameapishwa rasmi kuwa rais wa SITA wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Bi. Samia,61, amekulishwa kiapo Ijumaa Machi 19 na jaji mkuu Ibrahim Juma kwenye hafla iliyoandaliwa katika Ikulu iliyoko jijini Dar es Salaam.

Bi. Samia ambaye amekuwa makamu wa rais tangia mwaka 2015 atahudumu kipindi chote kilichosalia hadi mwaka 2025 kufuatia kifo cha rais John Pombe Magufuli.

Bi. Samia Suluhu Hassan ni mwanamke wa kwanza kushika nyadhifa hii nchini Tanzania na wa pili Afrika Mashariki.

Viongozi mbalimbali wanaendelea kumuomboleza Magufuli hasaa mchango wake katika kuleta umoja katika kanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na aliyejitolea kuwahudumia Watanzania.