Waziri wa Fedha katika kaunti ya Mandera Ibrahim Barrow amefariki baada ya kuugua ugonjwa wa corona.

Gavana wa kaunti hiyo Ali Roba amesema Barrow alifariki Ijumaa asubuhi baada ya kupatwa na ugonjwa huo.

Amesema marehemu alikuwa mfanyikazi aliyezingatia nidhamu na mchapa kazi wadhifa ambao ameshikilia kwa muda wa miaka minane.

Gavana Roba amewahimiza wakaazi wa kaunti hiyo na Wakenya kwa ujumla kuzingatia kwa umakini masharti ya usalama ili kuzuia msambao wa virusi hivyo.