Tume ya uchaguzi na mipaka IEBC imemtangaza Agnes Kavindu wa chama cha Wiper kama mshindi wa uchaguzi mdogo wa useneta kaunti ya Machakos.

Joyce Wamalwa afisa wa IEBC amemtangaza rasmi Kavindu kama mshindi na amemkabithi cheti cha kudhibitisha ushindi wake.

Kavindu ametangazwa mshindi baada ya kupata kura 104,080 akifuatiwa kwa umbali na Urbanus Ngengele wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) aliyepata kura 19,705.

Ngengele amekubali matokeo ya uchaguzi huo na kuaidi kufanya kazi na aliyeshinda uchaguzi huo.

Viongozi mbalimbali wamempongeza Kavindu kwa ushindi wake huku kiongozi wa chama cha Amani National Congress (ANC) akisema wakaazi wa Machakos wana imani naye.

Naye senata wa Elgeiyo Marakwet Kipchumba Murkomen amempongeza Kavindu huku akimkaribisha katika bunge la Seneti.

Kiti hicho kilisalia wazi kufuatia kifo cha Seneta Bonface Kabaka.