Matokeo ya upasuaji kwa mwili wa aliyekuwa naibu mkurugenzi wa mawasiliano katika tume ya ardhi nchini (NLC) Jennifer Wambua yameonesha kwamba aliuawa kwa kunyongwa.

Matokeo hayo yanayoonesha kuwa Wambua alinyongwa kwa kutumia mikono yamepewa familia na mpasuaji mkuu wa serikali Johannsen Oduor .

Wapelelezi wa idara ya DCI wanaendelea na uchunguzi kubaini hatua za mwisho za mwanahabari huyo kabla ya kukumbana na mauti yake.

Tayari wafanyikazi wenzake katika afisi za tume hiyo zilizoko Ardhi House wamehojiwa huku simu zake sawa na kamera za CCTV zikipigwa darubini.