Aliyekuwa mwanahabari wa NTV Winnie Mukami amefariki kutokana na matatizo yanayoambatana na corona.

Mukami ambaye pia alifanya kazi na shirika la habari la KBC hadi kifo chake alikuwa mwanachama wa bodi ya Kenya Pipeline (KPC).

Mukami ni mwanahabari wa pili kufariki wiki hii baada ya Robin Njogu wa shirika la Royal Media Services.

Waziri wa Ardhi Faridah Karoney amemuomboleza marehemu akiwataka Wakenya kuzingatia masharti ya usalama kuepuka msambao wa virusi vya corona ambavyo vinazidi kusababisha maafa.

Tasnia ya uanahabari vile vile inamuomboleza Jennifer Wambua aliyekuwa naibu mkurugenzi wa mawasiliano katika tume ya ardhi nchini NLC aliyepatikana ameuawa.