Mahakama kuu ya Machakos hii leo inatazamiwa kutoa uamuzi wa kesi inayolenga kuhalalisha ukeketaji wa wanawake nchini.

Jopo la majaji watatu Lydia Achode, Kanyi Kimondo na Margaret Muigai linatazamiwa kutoa uamuzi wa kesi hiyo mwendo wa saa nane unusu.

Mlalamishi Dr Tatu Kamau anaitaka mahakama kuwaruhusu wanawake walio na umri wa zaidi ya miaka kumi na nane kuamua iwapo wangependa kukeketwa au la.

Hata hivyo kesi hiyo imepingwa vikali na serikali na washikadau wengine ambao wanashikilia msimamo kuwa ukeketaji wa wasichana ni mila potovu iliyopitwa na wakati.

Madaktari na wanawake waliokeketwa pia waliielezea mahakama kuhusiana na madhara ya mila hiyo potovu na kuwataka majaji hao kutupilia mbali kesi hiyo.

Dr Tatu aliwasilisha kesi hiyo mahakamani tarehe 25 Julai mwaka 2017.