Mmoja wa mawakili wa aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko, Dkt John Khaminwa amejiondoa kwenye kesi ambapo gavana huyo wa zamani ameshtakiwa kwa ufisadi.

Dkt Khaminwa amejiondoa kwenye kesi hiyo kwa misingi kwamba hakimu wa mahakama ya kupambana na ufisadi Douglas Ogoti amekataa kuridhia ombi la kuhairisha kesi hiyo.

Haya yanajiri siku moja baada ya Sonko kumtaka hakimu Ogoti kujiondoa kwa hiyo akilalamikia maonevu.

Sonko analalama kuwa iwapo Ogoti ataendelea kusikiliza kesi dhidi yake, ataumia kwani hatapata haki.