Makamu wa rais wa Tanzania Samia Suluhu amesema kuwa rais John Pombe Magufuli anawasalimia sana Watanzania na anawasihi waendelee kuchapa kazi.

Akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Tanga, Mama Samia amewataka pia Watanzania kuacha kusikiliza maneno ya watu wa nje na kuwa na umoja katika wakati huu.

Kauli hii inajiri wakati kukiwa na uvumi katika mitandao ya kijamii kuhusu kutokuonekana kwa rais Magufuli.

Kufikia sasa, watu wanne wamekamatwa kwa tuhuma za kusambaza uvumi kwenye mitandao ya kijamii kuwa rais Magufuli anaumwa.

Mara ya mwisho kwa rais Magufuli kuonekanaka hadharani ilikuwa Jumamosi ya Februari 27,2021 hali amabayo imezua fununu na maswali kuhusu alipo na hali yake kiafya.