Madereva wa teksi zinaowapata wateja kwa njia ya mtandao wamelalamikia bei wanazotozwa na kampuni zinazomilki mitandao hiyo.

Wakiongozwa na Katibu Mkuu wa muungano wao Wycliffe Alutalala, madereva hao wamelalamikia bei za chini ambazo watejwa wao hutozwa na kusema zimeathiri pakubwa biashara hiyo.

Kuhusiana na ongezeko la bei ya mafuta, madereva hao wanasema hatua hiyo ni sawa na kuongewza msumari moto kwenye kidonda kwani imefanya kazi yao kuwa ngumu hata zaidi.