Sarah Wairimu anayedaiwa kumuua mumewe Tob Cohen amepata pigo baada ya mahakama kufutilia mbali ombi lake la kupinga kushtakiwa kwake.

Wairimu aliwasilisha kesi mahakamani Novemba mwaka jana kupinga mashtaka ya mauaji dhidi yake.

Jaji James Makau wa mahakama ya kikatiba ameamuru kuwa mahakama hiyo haina uwezo kusikiliza ombi hilo lililopingwa na upande wa mashtaka.

Amemshauri Wairimu kuwasilisha kesi hiyo katika mahakama kuu au mahakama inayoshughulikia maswala ya kifamilia.