Wakenya wapatao 4,000 wamepata chanjo dhidi ya ugonjwa wa corona kufikia sasa amesema katibu mkuu katika wizara ya afya Dkt.Mercy Mwangangi.

Akijibu maswali alipofika mbele ya kamati ya bunge la kitaifa kuhusu afya, Dkt. Mwangangi vile vile amewaambia wabunge kuwa kati ya waliopata chanjo hiyo, hakuna yeyote aliyeripoti kupata madhara ya kiafya.

Mwangangi aliyekuwa anawafahamisha wabunge kulikofikia shughuli ya kuwachanja Wakenya aidha amewaambia kwamba kuendelea kongezeka kwa idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini ni kiashirio kwamba taifa linashuhudia awamu ya tatu ya msambao wa virusi hivyo.