Kenya imeandikisha idadi kubwa ya maambukizi mapya ya corona pamoja na maafa huku waziri wa afya Mutahi Kagwe akitangaza kuwa taifa linashuhudia awamu ya tatu ya msambao wa virusi hivyo.

Waziri Kagwe amedhibitisha kuwa watu 713 wamekutwa na ugonjwa huo baada ya kupima sampuli 5,230 katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi ya visa hivyo 110,356.

Wagonjwa 12 zaidi wamefariki na kufikisha idadi ya maafa kuwa 1,898 huku watu 167 wakipona na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 87,903.

Wagonjwa 563 wamelazwa katika hospitali mbalimbali 98 wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi 28 wanasaidiwa ma mashine kupumua.