Mbunge wa Kabuchai Simiyu Kalasinga Majimbo ameapishwa rasmi kuanza majukumu yake baada ya kutangazwa mshindi kwenye uchaguzi mdogo ulioandaliwa Machi 4.

Kalasinga ameapishwa kwenye hafla iliyoongozwa na spika wa bunge la kitaifa Justin Muturi.

Kalasinga aliwania kiti hicho kupitia chama cha FORD K na alipata kura 19,274.

Kiti hicho kilisalia wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa eneo bunge hilo James Mukwe Lusweti.