Gavana wa Machakos Dkt. Alfred Mutua anamrai rais Uhuru Kenyatta kuitisha mkutano na viongozi wote wa kitaifa kujadili namna watakavyorejesha udhabiti kwenye siasa nchini.

Gavana Mutua anasema mkutano huo unafaa kuwajumuisha kinara wa chama cha ODM Raila Odinga pamoja na naibu rais William Ruto.

Mutua ambaye ametangaza kuwania urais kwenye uchaguzi mkuu ujao anahoji kuwa vurugu zilizoshuhudiwa kwenye chaguzi ndogo zilizokamilika juma lililopita ni taswira kamili ya hali itakavyokuwa kwenye uchaguzi mkuu wa 2022 ambapo taifa litasambaratika kwa sababu ya maslahi ya kisiasa.

Amesema mazungumzo hayo ya kitaifa yatawapa fursa viongozi kuwaelezea Wakenya watakachowafanyia iwapo wataingia katika nafasi za uongozi.