Peter Nabulindo wa chama cha Amani National Congress (ANC) ndiye mbunge mteule wa Matungu baada ya kumshinda mpinzani wake wa karibu na aliyekuwa mbunge na muwaniaji wa ODM David Were.

Nabulindo ametangazwa mshindi na tume ya uchaguzi na mipaka IEBC baada ya kupata kura 14,260 huku Were akipata kura 10,565.

Alex Lanya wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) alimaliza wa tatu kwa kupata kura 5,513.

Nabulindo amewashukuru watu wa Matungu kwa kumpa fursa ya kuwahudumia kama mbunge muda huu uliosalia.

Kiti hicho kilisalia wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge Justus Makokha Murunga.