Wakenya wametakiwa kujitokeza na kutoa maoni yao kuhusu mswada wa marekebisho ya katiba BBI ambao uko bungeni kwa sasa.

Makarani wa bunge la Senate na lile la kitaifa wamewataka Wakenya kutoa maoni yao kufikia Alhamisi wiki ijayo kwa kuyatuma kupitia maandishi au kufika binafsi mbele ya kamati ya haki na maswala ya kisheria.

Kamati hizo mbili zinatazamiwa kuandaa vikao vya umma kuhusu mswada huo wa BBI siku hiyo.

Ni mabunge matatu pekee ambayo yamekataa mswada huo kufikia sasa huku 43 yakiupitisha.