Tume ya huduma za walimu (TSC) imewataka wafanyikazi wake walioko kwenye likizo wakati huu kukatiza likizo na kurejea kazini Jumatatu ijayo kujiandaa kwa mitihani ya kitaifa.

Katika arifa, afisa mkuu mtendaji wa TSC Nancy Macharia amekatiza likizo zote kwa maafisa wa kaunti wakati wa mitihani hiyo.

Macharia ameeleza kwamba kurejea kuwa hii itahakikisha kuwa wafanyikazi wote wanasimamia mitihani hiyo na kuhakikisha kuwa mikakati yote ya kuzuia msambao wa virusi vya corona imefuatwa.