Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga ameendelea na ziara yake katika eneo la Pwani kwa kuzuru Mombasa hii leo.

Odinga aliyekuwa ameandamana na viongozi mbalimbali akiwemo gavana wa Mombasa Hassan Joho amehutubia wenyeji wa Kongowea ambapo amepigia debe mswada wa BBI.

Raila vile vile amesema kila mtu yuko huru kutuma maombi ya kuwania urais katika chama hicho ili wapambane katika mchujo.