Chanjo ya corona inatazamiwa kuanza kutolewa kote nchini Ijumaa hii baada ya rais Uhuru Kenyatta kuongoza shughuli ya usambazaji wake katika maeneo mbalimbali nchini.

Rais Kenyatta akiongoza usambazaji huo katika eneo la Kitengela ambako chanjo hizo zinahifadhiwa ameelezea matumaini yake kwamba zoezi la kutoa chanjo hiyo ikianza na wahudumu wa afya litafaulu.

Rais Uhuru Kenyatta vile vile amewasihi Wakenya wasieneze taarifa za uongo kuhusu chanjo hiyo huku akiwasihi kuendelea kuzingatia masharti ya usalama kuzuia msambao wa virusi vya corona.

Wakati uo huo, muungano wa madaktari wa kanisa katoliki wanawatadharisha Wakenya dhidi ya kukubali chanjo hiyo ya corona wakihofia usalama wake.

Hayo yakijiri

Watu 528 wamepatikana na virusi vya corona kutoka kwa sampuli 6,219 katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 107,329.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe katika taarifa amesema wagonjwa 185 wamepona ugonjwa huo na kufikifsha idadi ya waliopona kuwa 87,099.

Wagonjwa 4 zaidi wameaga na kufikisha idadi ya maafa nchini kuwa 1,870.

Wagonjwa 435 wamelazwa katika hospitali mbali mbali na wengine 1,583 wakishughulikiwa nyumbani.