Kampuni ya umeme ya Kenya Power imejipata pabaya huku maseneta wakiikemea kufuatua kupotea kwa stima kila mara katika maeneo mbalimbali nchini.

Maseneta wakiongozwa na Mutula Kilonzo Jr. wa Makueni wamesema shughuli za Wakenya wengi kujitafutia riziki zimeendelea kutatizika kwa sababu ya uzembe ya kampuni hiyo kushughulikia tatizo hilo.

Baadhi ya maseneta wameteta kuwa uzembe wa Kenya Power umesababishwa na kutokuwepo kwa ushindani kutoka kwa kampuni nyingine ya umeme.

Taarifa hiyo kuhusu kupotea kwa stima iliwasilishwa bungeni na Seneta wa Vihiga George Khaniri.