Mfanyibiashara mashuhuri anayedaiwa kuwalipa watu kumuua mwanawe Stephen Kinini Wang’ondu ameshtakiwa kwa mauji pamoja na watu wengine wanne.

Baba huyo pamoja na washtakiwa wenza akiwemo dereva wake James Mahinda, Eddy Kariuki, Raphael Wachira na Geoffrey Warutumo wamekanusha mashtaka dhidi yao mbele ya jaji Florence Muchemi.

Mahakama imeagiza washukiwa hao waendelee kuzuiliwa rumande kufuatia ombi lililowasilishwa na upande wa mashtaka.

Watano hao wanatuhumiwa kumuua Daniel Mwangi Wang’ondu,32, mkesha wa mwaka mpya katika kijiji cha Mwiyogo, Kieni kaunti ya Nyeri.