Bunge la kaunti ya Elgeyo Marakwet limekuwa la hivi punde kuangusha mswada wa marekebisho ya katiba BBI.

Spika wa bunge hilo Kiplagat Sabulei amesema madiwani 17 walipiga kura ya kupinga mswada huo dhidi ya 15 waliounga mkono.

Kaunti hiyo imekuwa ya tatu kukataa mswada huo baada ya Baringo na Nandi.

Wabunge wanatazamiwa kujadili mswada huo wakati wowote wiki hii baada ya maspika kupokea dhibitisho kutoka kwa mabunge 30 yaliyoidhinisha mswada huo.