Naibu rais William Ruto ameifariji familia ya mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri kufuatia kifo cha mwanao Arthur Kinyanjui.

Ruto kwenye ujumbe wake ameiombea familia hiyo faraja na kumuomba Mungu awape nguvu wakati huu wa msiba.

Athur,32, alifariki mapema hii leo akipokea matibabu katika hospitali ya Aga Khan, Mombasa baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Akidhibitisha taarifa hizo, mbunge huyo kupitia kwa mtandao wa Facebook amemwomboleza mwanawe huku akielezea hali ngumu wanayopitia kama familia.

Marehemu amkeuwa hospitalini tangia mwishoni mwa mwaka uliopita na inaripotiwa amekuwa akikumbwa na matatizo ya kupumua.