Waziri wa Usalama wa ndani Fred Matiang’i ameagiza kukamatwa kwa wanaume wote waliowapatia mimba wasichana wa shule zaidi ya 10,000 katika kaunti ya Trans Nzoia.

Akizungumza mapema Jumatatu wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika kaunti hiyo, Matiang’i amesema wanaume hao ambao wana umri wa zaidi ya miaka kumi na nane watafikishwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka ya ubakaji.

Matiang’i amepiga marufuku sherehe za usiku za matanga almaarufu kama ‘Disco Matanga’na kuwataka machifu na manaibu wao kuhakikisha kuwa hilo linatakelezwa.