Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga amekanusha madai kuwa anatumia mchakato wa marekebisho ya katiba BBI kuingia mamlakani kwa kutumia mlango wa nyuma.

Akihutubu kwenye mazishi ya aliyekuwa mbunge wa Bonchari Oroo Oyioka, Odinga amesisitiza kuwa kusudi lao ni kuhakikikisha kuwa Wakenya wameungana.

Amesisitiza kuwa mswada huo ni wa manufaa kwa mwananchi wa kawaida kupitia kuongezwa kwa mgao wa pesa za serikali za kaunti na hivyo kuwezesha maendeleo mashinani.

Na huku bunge likitazamiwa kuanza kujadili mswada huo wiki ijyao, waziri huyo mkuu wa zamani amewapongeza madiwa kwa kupitisa mswada huo kwa wingi.

Oyioka aliyefariki baada ya kuugua kiharusi amezikwa nyumbani kwake Suneka katika kaunti ya Kisii.