Mwakilishi wadi wa Karen kaunti ya Nairobi David Mberia amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela au alipe faini ya Sh700,000 baada ya kukutwa na hatia ya kupokea hongo ya Sh1.7M.

Akitoa uamuzi huo, hakimu wa mahakama ya kupambana na ufisadi Thomas Nzioki aidha amemuamuru diwani huyo asishikilie wadhifa wowote wa umma.

Mberia alishtakiwa kwa kupokea hongo ya Sh200, 000 kutoka kwa mfanyibiashara mmoja ili kumtetea kwenye uchunguzi uliokuwa unaendeshwa kuhusu umiliki wa kipande cha ardhi kinachomilikiwa na shule moja.

Diwani huyo alikuwa ameshtakiwa na wenzake Jared Okoth wa Mathare North na Ibrahim Njihia wa Woodley.

Hakimu huyo aliamuru kuwa upande wa mashtaka haukutoa ushahidi wa kutosha dhidi ya wawili hao na hivyo kuwaachilia huru.