Wakili Charles Kanjama amewasilisha kesi mahakamani kupinga shughuli ya kutathmini sahihi za mswada wa BBI iliyoendeshwa na tume ya uchaguzi na mipaka IEBC.

Kesi hiyo inatazamiwa kusikiliza Machi 8 huku Kanjama akitakiwa kuwapa wahusika kwenye kesi hiyo stakabadhi zinazohusiana na kesi hiyo kufikia kesho.

IEBC Jumatatu ilitangaza kuwa sahihi zilizoidhinishwa ni Milioni 3.1 kati ya sahihi Milioni 4.3 zilizowasilishwa kwake na kamati ya BBI.

Wakati uo huo

Kamati ya BBI imetangaza kuwa itaanza rasmi kampeini ya kupigia debe mswada wa BBI Jumatatu ijayo.

Mwenyekiti mwenza wa kamati hiyo Junet Mohammed amesema watabuni kamati mbalimbali kuongoza kampeini hiyo kote nchini.

INSERT: JUNET ON CAMPAIGNS

Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa chama cha ODM wataongoza kampeini hizo katika maeneo mbalimbali nchini.

Kamati hiyo vile vile imeitaka idara ya mahakama kushughulikia kesi zote zinazoambatana na mchakato huo wa BBI ili kuondoa kizingiti chochote katika maazimio ya kubadilisha katiba.