Mswada wa marekebisho ya katiba wa mwaka 2020 sasa utaamuliwa na wapiga kura kupitia kwa kura ya maamuzi baada ya kupata uungwaji mkono kutoka kwa zaidi ya mabunge ya kaunti 24.

Zaidi ya kaunti kumi na mbili zimepitisha mswada huo hii leo na kuongezea kwa kaunti kumi na mbili zilizokuwa tayari zimepitisha mswada huo wa BBI awali.

Kaunti ya hivi karibuni zaidi kupitisha mswada huo ni ile ya Tharaka Nithi, Kirinyaga, Nakuru, Meru, Nyandarua, Mombasa, ikifuatwa na Garissa, Lamu, Machakos, Nyeri na Kitui.

Kaunti zingine ambazo zimepitisha mswada huo leo ni Muranga, Bungoma, Taita Taveta, Nyamira, Makueni, Narok na Kakamega.

Madiwani waliopitisha mswada huo wameshabikia, miongoni mwa masuala mengine, kuongezwa kwa mgao wa pesa mashinani.

Mabunge yaliyopitisha mswada huo ni Samburu, Laikipia, Kajiado, West Pokot, Kisii, Nairobi, Trans Nzoia, Vihiga, Busia, Homabay, Kisumu na Siaya.