Wagonjwa 10 zaidi wameaga dunia kutokana na virusi vya corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi ya maafa nchini kuwa 1,837.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amethibitisha kuwa watu wengine 194 wameambukizwa ugonjwa huo na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 104,500.

Idadi ya waliopona imeongezeka na kufikia 85,665 baada ya wagonjwa wengine 39 kupona.

Wagonjwa 344 wamelazwa katika hospitali mbalimbali nchini, 55 wakiwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi 23 wakisaidiwa na mashine kupumua.