Inspekta mkuu wa Polisi Hillary amewatetea maafisa wake dhidi ya shutuma kwamba wanatumiwa visivyo kukabiliana na wapinzani wa kisiasa.

Mutyambai akijibu maswali kutoka kwa wananchi kupitia kwa mtandao wa kijamii wa Twitter amesema Polisi hawampendelei yeyote na hawana msimamo wa kisiasa.

Ameongeza kuwa jukumu kuu la Polisi ni kuwalinda raia na kuzuia mkutano wowote ambao huenda ukasababisha vurugu.

Majibu wa Mutyambai yanajiri wakati ambapo naibu rais William Ruto na wendani wake wamekuwa wakiwatuhumu Polisi kwa kutumiwa vibaya kutatiza mikutano yao.