Polisi wamewakamata tena mwenyekiti wa shirika la kutetea haki za kibinadamu la MUHURI Khelef Khalifa pamoja na mwenzake Francis Auma.

Wawili hao wameshikwa muda mfupi baada ya mahakama kuwaachilia huru ambapo walishtakiwa kwa kutatiza amani na kuzua vurugu.

Hata hivyo Khelef na Auma walikanusha mashtaka dhidi yao.

Polisi hawajatoa maelezo kuhusu kukamatwa tena kwa wanaharakati hao.

Wawili hao walikamatwa Alhamisi kwa kushiriki maandamano kupinga matumizi ya MPESA kulipia huduma za kivukio cha Likoni.