Rais Uhuru Kenyatta amewatahadharisha Wakenya dhidi ya kukubali kupigana kwa sababu ya wanasiasa.

Akizungumza katika maeneo ya Kayole  na Dandora  jijini Nairobi alipokuwa anazindua miradi mbalimbali ya maendeleo, rais Kenyatta amewataka Wakenya kudumisha amani maanake uongozi unatoka kwa Mungu.

Kenyatta vilevile amepigia debe mchakato unaoendelea wa BBI huku akilipongeza bunge la kaunti ya Nairobi kwa kupitisha mswada huo.

Rais Kenyatta aidha ameahidi kuwa mpango wa“Kazi Mtaani” utarejea hivi karibuni ili kuwanufaisha vijana wasiokuwa na ajira.