Miswada miwili ya marekebisho ya katiba kupitia kura ya maamuzi inatazamiwa kujadiliwa katika vikao vya bunge la kitaifa asubuhi.

Wabunge wanatazamiwa kujadili mswada wake mwakilishi wa wanawake kaunti ya Busia Florence Mutua na mbunge wa Ndia George Kariuki.

Haya yanajiri huku kaunti SABA zikiwa zimepitisha mswada wa marekebisho ya katiba BBI kufikia sasa.

Kaunti hizo ni pamoja na Kajiado, Trans Nzoia, Pokot Magharibi, Busia, Homa Bay, Kisumu na Siaya.

Hii inamaanisha kwamba mswada huo unahitaji kuungwa mkono na kaunti 17 pekee ili kuwasilishwa bungeni na kisha kura ya maamuzi.

Kufikia sasa,bunge la kaunti ya Baringo ndilo la kipekee kupinga mswada huo.

Mswada huo unahitaji kuungwa mkono na mabunge ya kaunti yapatayo 24 kati ya 47 ili kufanikisha mabadiliko ya sheria.